7 Oktoba 2014 - 20:26
Nchi zipi zinazoipa silaha kikundi cha kigaidi cha Daesh?

Ripoti za mashariki ya kati zinaonyesha kuwa Daesh ndio wanunuzi bora wa silaha kutoka katika nchi zenye viwanda vikubwa vya kutengeza silaha duniani, nao wanamiliki aina za silaha kutoka nchi 21

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: silaha nyingi wanazo zitumia magaidi wa Daesh ni kutoka katika nchi ya Marekani, Urusi na China. Daesh kunako suala la kununua silaha hawana tatizo lolote, kwani kiasi kikubwa cha silaha wanazipata kutokana na ngawira za vita na nyengine kununua katika mataifa hayo makubwa duniani.
Kwa upande mwingine mapato ya Daesh yanayotokana na mafuta wanayopata magaidi hao katika sehemu wanazomiliki nayo ndio  miungoni mwa asilimali kubwa inayowaingizia pesa nakuweza kununua silaha hizo kutoka katika mashirika makubwa ya kutengeza silaha katika nchi za Marekani na Ulaya.
Ripoti hii ikieleza kuwa silaha ziliopo mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh zinatoka nchi 21 dunia, ama mashirika makubwa zaidi yanayooza silaha hizo kwa magaidi hao ni mashirika ya kimarekani, kito ambacho kinaleta mshangao kutoka kwa utawala wa Marekani kwa kuvunga kuwa utataka wake unataka kupigana na magaidi wa Daesh, hali yakuwa silaha walizo nazo magaidi hao ni kutoka mikononi mwao.